Wednesday, February 12, 2014

MKUU WA SHULE AKIGAWA ZAWADI MBALIMBALI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YAO YA MWAKA 2013

Mwanafunzi aliyeongoza kwa ufaulu kwa mwaka 2013 akiwa kidato cha kwanza akipata zawadi zake kutoka kwa mkuu wa shule.

Zoezi la ugawaji wa zawadi wafaulu likiendelea kutoka kwa mkuu wa shule na ofisi ya taaluma.

Wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2013 walioongoza kwenye ufaulu wa masomo yao wakiwa wamekumbatia zawadi zao.


Wanafunzi wa kidato cha pili nao hawakuwa nyuma katika kujipatia zawadi zao baada ya kufanya vizuri ktk mtihani taifa wa kidato cha pili mwaka 2013.

Kazi ya ugawaji zawadi ikiendelea kwa wanafunzi wa kidato cha pili.

Waliofanya vizuri katka masomo mbalimbali katika mtihani wa taifa wa kidato cha pili wakiwa na zawadi zao.

Kidato cha tatu mwaka 2013 nao hawakubaki nyuma katika upokeaji wa zawadi baada ya kufanya vizuri.

Hongera sana ndilo neno lililotawala kwa wanafunzi hawa huku wakifurahia zawadi zao.


Wanafunzi wa kike walikuwa vinara kaitka ufaulu hasa kwa kidato cha tatu mwaka 2013, Wakiwezeshwa kweli wanaweza.

Pia wanafunzi wa kidato cha tano hawakuwa mbali katika kuzipokea zawadi hizo ambazo zimeonge hari ya wanafunzi kujisomea kwa bidii katika masomo yao.

Pongezi kutoka walimu wao wa masomo inatia hamasa kubwa kwa walimu na wanafunzi pia.

"Ahsante mkuu nitaongeza juhudi zaidi" ni neo la mwanafunzi mara baada ya kuwa mmoja wa wafaulu, kweli ni raha tupu ukiwa Nyerere High School - Migoli.

No comments:

Post a Comment

Designed by: Hatibu Juma, Email: hatibu.jayjay@gmail.com, Cell phone: +255 755 638 028.